Tuesday, September 6, 2016


Kamsemo ambako kalikuwa kananitia moyo na kuendelea kufikiria ajira tu peke yake wakati maisha hayabadiliki ni haka "maisha hayana formula banah" kiukweli msemo huu ulikuwa unanifanya nijione kuwa ipo siku nitafanikiwa kwa miujiza, lakini muda fulani nilikuwa naona haina haja kujihangaisha kwasababu nimeshaambiwa maisha hayana formula(kanuni) sasa kilichonistua ni kuwa umri unakwenda miaka inapita nikaanza kustuka nikaanza kujiuliza kama maisha hayana kanuni mbona vijana wenzangu wanabadilisha maisha yao wakati mimi niko hapa hapa, mbona Kuna vijana kama mimi wanavipaji vyao na hawahangaishwi na ajira hahahaaaa nikagundua nimebeba mzigo kichwani kwangu kale kausemi kuwa maisha hayana formula, usemi huu umewafanya vijana wengi sana na hata ambao sio vijana kusema ipo siku nitafanikiwa tu halafu kulala ndani.
Usemi huu umewafanya vijana wengi kuendelea kukaa vijiweni wakipiga story wakitiana moyo kizembe eti ipo siku maisha yatakuwa mazuri wakati wapo kijiweni, usemi huu umewajaza nyumbani vijana ambao wamemaliza Chuo wakiamini ipo siku watapata ajira tu kwasababu maisha hayana kanuni wamesahau kujiajiri, hakuna mafanikio ya bahati mbaya, kama na wewe bado umekariri maisha hayana kanuni leo nakwambia futa huo usemi kichwani Kwako maisha yana kanuni zake ambazo kama kweli unataka kufanikiwa lazima ukubali kuzifata kama hauko tayali utaendelea kuwa mkia siku zote za maisha yako.
KUSEMA MAISHA HAYANA KANUNI NI UVIVU WA KUFIKIRIA
,

Kanuni ya kufanikiwa kuwa mjasiriamali ni kuanza kuhudhuria mafunzo na semina mbalimbali za ujasiriamali usipofanya hivyo utasikia mafanikio kwa jirani watu ninaowafundisha kutoka kwenye ajira hadi kujiajiri nawaambiaga hili,sasa usidhani utapata mafunzo haya bure, kama hauko tayali kulipia gharama za mafanikio yako endelea kusema maisha hayana formula, kanuni ya kufanikiwa katika sehem uliopo ni kutenda bila kuogopa na kukata tamaa, sasa unamkuta mtu kaonyeshwa fursa unamsikia nitafanya kesho, endelea kuahirisha tu, mwingine ameingia kuanzisha kitu siku mbili anataka kufanikiwa, asipofata kanuni ya uvumilivu na kutokukata tamaa hata kama atashindwa mara ngapi halafu anataka maisha mazuri imekula Kwake. Maisha yanakanuni zake ukizifuata utafanikiwa, endelea kufatulia makala hizi siku moja tafundisha.
USIPOKUWA TAYALI KUZITAFUTA NA KUZIFATA KANUNI ZA MAISHA, MAISHA MAZURI UTAYASIKIA KWA JIRANI
USIKATE TAMAAA KATIKA MAISHA
 
*** JITAMBUE **

The right action = Success
Nicheki whatsapp -
0767962720 / 0717962720


Ni matumaini yangu mu wazima wa afya wapenzi wasikilizaji, na karibuni kujumuika nami katika makala nyingine ya Ijue Afya Yako. Wiki iliyopita tulizungumzia usafi wa kinywa, umuhimu wake na pia jinsi ya utunzaji wa fizi na meno. Bado tunaendelea kujadili suala hilo ambapo leo tutazunguzia maradhi mbalimbali ya fizi na meno na namna ya kuyazuia. karibuni.

Aina za maradhi ya fizi na dalili zake

Kupiga mswaki na kutunza meno sio suala gumu na iwapo tutapiga mswaki ipaswavyo pamoja na kutumia nyuzi kusafisha katikati ya meno, tunaweza kuzua maradhi ya fizi na pia meno kuoza. Maradhi ya fizi husababishwa na utando kwenye meno unaotengenezwa na bakteria, ute na chembechembe nyinginezo zinazoganda kwenye meno. Kwa mujibu wa Taasisi ya Meno ya Marekani (ADA) iwapo utando katika meno hautaondolewa huwa mgumu na kuwa ugwagwa wa meno au tarter inayotumiwa na bakteria. Mchanganyiko wa utando na ugwagwa katika meno husababisha uvimbe kwenye fizi hali inayojulikana kitaalamu kama gingivitis. Ukoga wa meno au ugwagwa unaweza kundolewe na daktari wa meno au dentist.

Maradhi ya fizi yana awamu tatu. Awamu ya kwanza kama tulivyosema ni gingivitis, ambapo fizi huwa nyukundu, huvimba na hutokwa na damu kwa urahisi. Iwapo hali hiyo itagundulika mapema inaweza kutatuliwa kwa kupiga mswaki vizuri na kutumia nyuzi kusafisha katikati ya meno.

Awamu ya pili ya ugonjwa wa fizi ni hali ijulikanayo kama Periodontitis ambapo uvimbe hutokea kuzunguka jino. Awamu hii ni iliyoendelea zaidi ya ugonjwa wa fizi inayotokea wakati sumu ya bakteria katika utando inapoharibu fizi zilizoshikilia jino. Suala hilo husababisha fizi ziachane na jino na kutengeneza mada haribifu. Baadhi ya wakati mfupa ulioliwa kuzunguka jino unaweza kuonekana. Matibabu ya maradhi haya ya fizi ni muhimu sana ili kuzuia mmomonyoko wa mfupa na kung'oka meno.

Awamu ya tatu ya maradhi ya fizi ni periodontitis iliyoendelea. Katika steji hii uharibifu wa fizi huwa mkubwa zaidi kuliko kabla na mfupa wa jino hulika. Pia meno huweza kung'oka na baadhi ya wakati huhitaji kung'olewa iwapo matibabu hayatosaidia.

Dalili za maradhi ya fizi

Hapa linajitokeza swali kwamba ni zipi dalili zinazojitokeza wakati mtu anapokuwa na ugonjwa wa fizi ulioendelea? Dalili za advanced periodontitis ni kuwa na harufu mbaya ya mdomo ambayo haiishi. Fizi kuvimba, kuwa nyekundu na laini. Dalili nyingine ni fizi kusogea mbali na meno, kuhisi maumivu wakati wa kutafuna na kupoteza hisia katika meno.

Sababu za maradhi ya fizi

Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kumfanya mtu awe katika hatari ya kupatwa na magonjwa ya fizi. Miongoni mwa sababu hizo ni kuvuta sigara au kutafuna tumbaku. Mbali ya kuwa uvutaji sigara unaathiri mwili wa binadamu kwa njia tofauti, moja ya athari za ufutaji sigara hudhihirika katika kinywa cha mtu. Kwa kuwa moshi wa sigara hupita kwenye meno na fizi, kinywa cha mvuta sigara huwa kituo cha nicotine ambayo huharibu muonekano wa meno kwa kuyabadilisha rangi na kuacha harufu mbaya kinywani. Si hayo tu bali uvutaji sigara pia huathiri tishu za fizi na kupunguza mtiririko wa damu katika fizi, na kuleta uharibifu unaosababisha fizi zisogee mbali na meno.

Wataalamu wanatuarifu kuwa, asilimia 75 ya watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fizi ni watu wazima huku wale wanaovuta sigara wakiwa kwenye hatari ya kusumbuliwa na ugonjwa huo mara 7 zaidi ikilinganishwa na watu wasiovuta sigara.

Sababu nyingine inayochangia katika kupata ugonjwa wa fizi ni mabadiliko ya homoni kwa wasichana na wanawake. Wanawake wako katika hatari zaidi ya kupata matatizo ya kinywa na meno kuliko wanaume kutokana na mabadiliko ya homoni yanayosababishwa na maumbile yao. Sio tu mabadiliko ya homoni kwa wanawake na watoto huathiri mtiririko wa damu katika tishu za fizi, bali pia huchangia katika suala zima la kupatikana ugando kwenye meno au plague unaosababisha meno kuoza. Mabadiliko ya homoni huwafanya wanawake wawe kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa fizi wanapokuwa katika hali tofauti kwenye maisha yao ambazo ni wakati wa kubalehe, wakati wa hedhi, wanapotumia vidonge vya kuzuia mimba, wanapokuwa wajawazito na wakati wanapoacha kupata hedhi yaani menopause. Hayo yote husababishwa na mabadiliko yanayoshuhudiwa katika homoni za estrogen na progesterone kwenye vipindi hivyo. Kwa sababu hiyo tunaweza kusema kuwa, watoto wa kike, wasichana na wanawake kwa ujumla wanapaswa kuzingatia zaidi usafi na utunzaji wa fizi na meno ili kuepusha uharibifu wa meno unaowapata zaidi kutokana na jinsia yao kuliko wanaume.

Sababu nyingine inayoweza kumfanya mtu apatwe na maradhi ya fizi ni ugonjwa wa kisukari. Madaktari wanatuambia kuwa, watu walio na ugonjwa wa kisukari ambao hawadhibiti vyema ugonjwa huo, wako katika hatari zaidi ya kupata matatizo ya meno na maambukizi katika fizi. Hii ni kwa sababu ugonjwa wa kisukari hupunguza mtiririko wa damu kwenye fizi na pia kiwango cha juu cha sukari kwenye damu husababisha kinywa kiwe kikavu na kuzidisha ugonjwa wa fizi. Upungufu wa mate mdomoni huongeza bakteria wanaoharibu meno na kuleta utando. Iwapo mtu mwenye kisukari atadhibiti ipasavyo kiwango cha sukari kwenye damu, hatari ya kupata matatizo ya meno hupungua.

Namna ya kuzuia maradhi ya fizi

Suala muhimu zaidi linaloweza kuzuia mtu asipatwe na maradhi ya fizi na kuoza meno ni kupiga mswaki na kutumia nyuzi kuondosha uchafu katikati ya meno kwa uchache mara moja kila siku. Suala hilo linaweza kuzuia maradhi ya fizi, meno kutoboka na kung'oka. Licha ya kusafisha meno kila siku, jambo jingine muhimu ni kufanyiwa uchunguzi na daktari wa meno kwa uchache mara moja kwa mwaka. Hii ni kwa sababu hata kama tunajitahidi kwa kiasi gani kupiga mswaki, lakini mgando na ugwagwa hujitokeza na kusababisha matatizo katika fizi.

Je, ni namna gani tupige mswaki kwa njia iliyo sahihi?

Kwanza kabisa tunashauriwa kupiga mswaki asubuhi na kabla ya kwenda kulala. Ikiwezekana piga mswaki baada ya kula chakula. Kama hauwezi, piga mswaki baada ya kula vyakula vya sukari. Tunapaswa kutumia mswaki laiini na wa wasitani, kwani mswaki mkubwa hautafika kwenye meno ya nyuma ilhali ule ulio mdogo utakufanya utumie wakati mwingi sana katika kusugua meno. Ikiwa unahitaji usaidizi katika kuchagua mswaki, pata ushauri kutoka kwa daktari wako wa meno. Tumia dawa ya meno iliyo na floraidi. Watoto wanapaswa kutumia kiasi kidogo cha dawa ya meno na watu wazima watie dawa ya meno kulingana na urefu wa nywele za mswaki.

Wataalamu wanatushauri kubadilisha mswaki pindi ule tunaotumia unapochoka, kila baada ya miezi mitatu au minne. Pia tunashauri kuwa ni vizuri kubadilisha mswaki mpya kila baada ya kupata mafua, uvimbe katika koo na magonjwa mengineyo kama hayo.

Kumbuka kusugua pande zote za meno kwa njia ifuatayo:

Sugua meno yako polepole bila kutumia nguvu kutoka sehemu ya nyuma hadi mbele. Sugua karibu na ufizi kwa mwendo wa mviringo, ili mswaki ufike sehemu ambapo meno na ufizi zinakutanika mahali ambako chembechembe za chakula hujificha.Sugua sehemu zote za meno, sehemu ya nje, sehemu ya kutafunia chakula na sehemu ya ndani ya meno.Tumia sehemu ya juu ya mswaki kusafisha sehemu ya ndani ya meno ya juu, kwa mwendo wa juu na chini.Sugua ulimi wako kwa upole ili kuondoa vijidudu au viini vinavyosababisha harufu mbaya.Sukutua na hifadhi mswaki wako sehemu nzuri na salama kwa matumizi ya baadaye.

Naaam wapenzi wasikilizaki, na kufikia hapo basi hatuna la ziada kwa leo, hadi wiki ijayo tudumishe afya zetu.

Friday, December 4, 2015

Nini maana ya ulcers?
Ulcers  ama vidonda vya tumbo ni michubuko ama vidonda vinavyotokea kwenye njia ya mfumo wa chakula hasa mfuko wa tumbo (stomach)na sehemu ya awali ya utumbo mwembamba (duodenum).


Ni nini husababisha ulcers?
Kwa kawaida mwili hutengeneza asidi na homoni mbalimbali kwa ajili ya kusaidia mmeng’enyo wa chakula kwenye mfuko wa chakula k.m HCL na Gastric juice. Vimelea hivi vikizidi husababisha michubuko au kudhoofisha kuta za ndani ya tumbo na hivyo kuongeza hatari ya mtu kupata vidonda vya tumbo


 ****Maambukizi ya bakteria aina ya  Helicobacter pylori husababisha mtu aliye kwenye hali hiyo kupata vidonda vya tumbo.****
 

Mwili hujikinga dhidi ya asidi ya tumboni kwa:
Kuruhusu chakula kisafiri kwa spidi inayostahili 
Kutengeneza alkali ili kuleta uwiano na asidi iliyotengenezwa tumboni hivyo chakula kilicho katika utumbo mwembamba huwa hakina asidi wla alkali. 
 Vitu hatarishi vinavyoweza kupelekea vidonda vya tumbo ni nini?
Msongo wa mawazo (stress)
Vinywaji vyenye caffein kama kahawa 
Sigara(nicotine) 
Pombe
Kutokuwa na uwiano sahihi wa kula chakula k.m kula kupitakiasi usiku kwa sababu mchana ulishinda njaa. 
Magonjwa k.m ini 
Kutumia dawa hasa za NSAIDs k.k aspirin 
 Dalili za vidonda vya tumbo
Mara nyingi hutokana na eneo kilipo kidonda
 Mfuko wa tumbo(gastric) 
 - maumivu makali ya tumbo saa1-2 mara baada ya kula
Mwanzo wa utumbo mwembamba (duodenum)
-maumivu makali ya tumbo kabla ya kula (hupungua pale unapokula au maziwa)
-maumivu makali ya tumbo usiku wa manane
Dalili za jumla
-kupungukiwa na damu mwilini
-choo kuwa na rangi nyeusi(melena) 
 -kutapika damu (haematemesis)

  -kukosa hamu ya kula

  -kuwa na kiungulia

  -maumivu ya kifua


Dalili za hospitali
-kuuma tumbo akiguswa 
 -tumbo kuunguruma (succission splash) 
- H pylori wakiotesha damu 
 Madhara ya vidonda vya tumbo
Kwa watoto ni utapiamlo

Kutoboka kwa utumbo

Maambukizi ya bakteria wengine kupitia katika kidonda

Kupungukiwa damu

Kupungukiwa uzito

Vidonda kupeleka magonjwa mengine kama gastric outlet obstruction(GOO)
Matibabu 
Matibababu ya madawa ya hospitali  
  mgonjwa hupewa dawa hospitali za kupunguza asidi na kuua bacteria wa H pylori. Kidonda hubaki kwa muda mrefu k.m omeprazole, flagyl na amoxicilin kwa walau wiki mbili.
Matibabu ya upasuaji hospitali 
Hii ni kwa baadhi ya wagonjwa ambao vidonda vyao ni sugu, vikubwa vyenye hatari ya kutoboa 
utumbo 
 Matibabu asilia ya vidonda vya tumbo
       •Matibabu asilia ya vidonda vya tumbo inahusisha virutubisho mbalimbali muhimu kwa ajili ya kuleta uwiano wa asidi mwilini, kuua bakteria wa H pylori na kuponya vidonda vyenyewe pamoja na mabadiliko kwa mtazamo wa maisha bora zaidi.
 Mgonjwa wa vidonda vya tumbo afanye yafuatayo:
Kunywa maji safi na salama lita 2-3 
Kupunguza matumizi ya kahawa yenye caffeine 
Kuepuka kula mlo mmoja mwingi baada ya kukosa mingine k.m usiku 
Epuka vyakula vinavyokuletea aleji 
Asinywe pombe 
Kutotumia dawa kama za NSAIDs kama aspirini
Asivute sigara 
Ale chakula kwa wastani kwa vipindi 
Asitumie dawa za NSAIDs kama aspirini 
Atumie virutubisho muhimu vya asilia kwa ajili ya ugonjwa 
wake wa vidonda vya tumbo
 Virutubisho muhimu kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo
Mgonjwa wa vidonda vya tumbo anakabiliwa na: 
  - maambukizi ya bakteria wa H pylori 
  - kuta dhaifu za tumbo 
  - vidonda katika tumbo
- upungufu wa damu 
 PATA VIRUTUBISHO MUHIMU KWA AJILI YA TATIZO HILO
PHONE: =+255717962720
               = +255767962720

Mr.Mputa

You are welcome in this blog you ca get us through..
Mobile+255717962720
+255767962720
Njombe Iringa Tanzania

TANGAZO

Karibuni katika Blog ya Jiliwaze hapa utapata mambo mbali mbali yakufunza na kuonya na kama unahitaji kutengenezewa email,facebook ac,page ama blog wasiliana nasi kupitia.. Phone:0717962720/0767962720 Email:mputae@yahoo.com :mputae@rocketmail.com

Popular Posts