Friday, December 4, 2015

Ni vimbe ambazo hutokea katika sehemu za uzazi wa mwanamke.
Ni vimbe zinazotokea katika kizazi (uterus). Vimbe hizi hazimaanishi kuwa ni kansa.
zinatengenezwa na kambakamba zilizofungamana (muscle fibre)
Fibroids huanza kwa ukubwa kama wa njegere, lakini huweza kukua kwa ukubwa wa tikiti maji.
Inakadiriwa kwamba asilimia kati ya 20-50% ya wanawake wana hili tatizo au watakuwa na hili tatizo katika kipindi Fulani cha maisha yao.
Fibroids hupatikana zaidi kwa wanawake wenye umri kati ya miaka 30-40 na hupungua ukubwa mara baada ya umri wa utu uzima.
Uchunguzi uliofanyika huko marekani unaonyesha kwamba Fibroids huwapata wanawake wa kiafrika mara tisa zaidi ya wanawake wazungu. Sababu yake haijulikani.

NINI KINASABABISHA FIBROIDS?
Ingawa sababu/chanzo hasa cha Fibroids hakijulikani, utafiti unaonyesha kwamba fibroids huchochewa na oestrogen mwilini.
Mara nyingi fibroids hukua kwa mwanamke pale ambapo kiwango cha oestrogen kimeongezeka mwilini, na pia fibroids hupungua pale ambapo kiwango cha oestrogen nacho kikipungua.

 OESTROGEN NI NINI?
*Ni mkusanyiko wa homoni ambazo ndizo zinazoukuza mwili wa mwanamke kijinsia, mfano ukuaji wa viungo kama matiti na kupata hedhi.
*Pia,wanawake ambao wana uzito zaidi ya kg.70 wana hatari kubwa zaidi ya kupata fibroids, pia hii ni kutokana na kiwango kikubwa cha oestrogen katika umri huu..
*Wakati wa zamani, Fibroids ingeweza kusababishwa na matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango. Hii ni kwasababu vidonge hivi vilikua na kiwango kikubwa cha oestrogen.
*Lakini kwa hivi sasa,vidonge hivi vya uzazi wa mpango havina kiwango kikubwa cha oestrogen kama ilivyokuwa hapo awali.

 AINA ZA FIBROIDS
Fibroids zinatofautishwa kutokana na sehemu ambapo imetokea.
Yapo makundi mawili yanayoweza kugawanya aina za fibroids. 1)Fibroids zinazotokea ndani ya mji wa mimba,
2)Fibroids zinazotokea kwenye kuta za nje ya mji wa mimba. DALILI ZA FIBROIDS
Inakadiriwa kwamba, asilimia 75% ya wanawake wenye fibroids hawana dalili zozote na wala hawajui kama wana fibroids.
Kuweza kujua dalili za fibroids, inategemea na ukubwa wa fibroid na wapi zilipo kwenye kizazi. Hii pia inachangia aina ya dalili atakazopata mtu.
Mfano: Fibroid ndogo ambayo ipo kwenye kuta za kizazi, haitakuwa na dalili sawa na Fibroid kubwa inayoota kuelekea nje ya kizazi.
-Dalili kubwa inayofahamika ni ile ya kutokwa na damu nyingi sana wakati wa hedhi.

Dalili nyingine ni kama,
-Maumivu ya tumbo,
-Inaathiri mfumo wa haja.(kubwa na ndogo)
-Kuhisi mkojo mara kwa mara
-Mkojo kutoka kdogokidogo/kuvuja
-Mkojo kushindwa kutoka kirahisi.
-Kukosa choo.(constipation)
-Kuwa tasa.(kutoshika ujauzito)
-Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Wakati wa kujifungua, kama fibroid itakuwa kwenye njia ya kutolea mtoto inaweza kusababisha damu nyingi kutoka, au ikishindikana mama hufanyiwa upasuaji ili kumtoa mtoto.

MATIBABU YA FIBROIDS (HOSPITALI)
Zipo njia kuu mbili za kihospitali za kutibu fibroids.
-Kutumia dawa (drug treatment)
-Kufanyiwa upasuaji (surgical procedures)

1. KUTUMIA DAWA
*Mkusanyiko wa dawa zijulikanazo kama GnRH analogues hupunguza kiwango cha oestrogen mwilini na hivyo kusababisha firoid kusinyaa.
*Uchunguzi unaonyesha kwamba, dawa hizi zikitumika kwa miezi sita hupunguza ukubwa wa fibroid kwa asilimia 50%
*Pia dawa hizi husitisha mzunguko wa mwezi (hedhi).
*Inashauriwa kwamba matumizi ya dawa hizi (GnRH analogues) yasitumike zaidi ya miezi sita kwani dawa hizi huweza kuleta madhara makubwa.
*Pia, mara baada ya kuacha kutumia dawa hizi, wiki chache baadae fibroids huanza kukua tena, na mwanamke huanza kupata hedhi tena kama awali,ikiambatanisha na maumivu makali.
*Kwa baadhi ya wanawake huwa hawapati tena hedhi hadi kifo.

2. KUFANYIWA UPASUAJI
Upasuaji unahusisha mambo yafuatayo.
Kuiondoa fibroid yenyewe na kuacha kizazi (Myomectomy)
Kukiondoa kizazi kabisa (Hysterectomy)
Kuzuia damu kwenda kwenye fibroids (Uterine artery embolisation)
*Ipo njia ambayo haijazoeleka sana, ambayo mtu huchomwa sindano nne tumboni zikielekea ilipo fibroids kwa ajili ya kuiua kwa kemikali maalum.


 KUNA NJIA YA KUONDOA UVIMBE BILA KUFANYIWA OPERATION AMA KUTUMIA MADAWA AMBAYO NAYO SI MAZURI KWA KUTUMIA VIRUTUISHO/LISHE BORA
*Aloe vera Gel
Aloe vera inayo madini mengi ikiwemo vitamin B 12 za aina zote ambayo husaidia kuongeza damu. Pia Aloe vera yenyewe ina uwezo wa kuzuia kutokwa kwa damu,na kuzuia vimbe za aina yoyote kwahiyo ukimpa mtu mwenye fibroids zile vimbe zinayeyuka.Pia ni Lishe kamili hivyo husaidia kutunza ngozi ya yule mgonjwa na kuiweka katika hali ya kuwa na afya zaidi.
*Aloe Berry Nectar
Mbali na kuwa na alovera yenye virutubisho vingi vinavyosaidia kujenga mwili, pia ina matunda aina ya Cranberries ambayo huondoa kabisa vimbe za kwenye kizazi. Pia ina madini ya chuma ambayo yanasaidia katika kurudisha damu iliyopotea kwenye hedhi ya muda mrefu
*ARCTIC SEA
Omega -3 Inayopatikana kwa samaki aina ya ‘Salmon” inazuia uwezekano wa kukua kwa fibroids baada ya kukatwa.
inasaidia katika kudhibiti ongezeko la Estrogen ambayo ikiwa nyingi mwilini inaweza kusababisha vimbe kutokea kwenye kizazi. Pia inapunguza maumivu wakati wa hedhi.
*NATURE MIN.
Kutokana na kupoteza damu nyingi wakati wa hedhi Madini ya Iron mengi yanapotea katika kipindi hiki hivyo mgonjwa wa fibroids anahitaji kupata madini mengi ya Iron ili kuongeza chembe chembe za damu mwilini

KAMA UNATATIZO HILO UMEPATA UFUMBUZI JALI AFYA YAKO NA WANAOKUZUNGUKA PATA LISHE YA KUYEYUSHA UVIMBE HUO BILA OPERATION
 PHONE  0717962720
                0767962720 

0 comments:

Post a Comment

Mr.Mputa

You are welcome in this blog you ca get us through..
Mobile+255717962720
+255767962720
Njombe Iringa Tanzania

TANGAZO

Karibuni katika Blog ya Jiliwaze hapa utapata mambo mbali mbali yakufunza na kuonya na kama unahitaji kutengenezewa email,facebook ac,page ama blog wasiliana nasi kupitia.. Phone:0717962720/0767962720 Email:mputae@yahoo.com :mputae@rocketmail.com

Popular Posts