Friday, February 24, 2012



Saturday, 25 February 2012 08:45
Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo
Elias Msuya na Leone Bahati
MBUNGE wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo ametakiwa kuripoti katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ifikapo Machi 7 mwaka huu, ili kusikiliza hukumu ya kesi ya madai inayomkabili.

Shelukindo anadaiwa kushindwa kulipa mkopo aliouchukua kutoka kwenye benki ya Azania mwaka 2005.
Hakimu wa mahakama hiyo, Joyce Minde alisema hukumu ilishatolewa na mahakama hiyo ambayo ilimamuru Shellukindo kulipa deni analodaiwa na benki hiyo, lakini hadi sasa ameshindwa kutekeleza amri hiyo.

“Hiyo kesi siyo ngeni, ni kesi ya madai namba 92 ya mwaka 2005 na ilishatolewa hukumu. Tunachofanya sasa ni kukazia hukumu tu,” alisema Minde na kuongeza:

“Kuna njia mbalimbali za kukaza hukumu kama vile kukamata mali za mdaiwa, mfano nyumba au kufungwa jela.”
Alisema; “Nitasikiliza utetezi wake na nitatoa hukumu kulingana na uzito wake. Kama hauna uzito mahakama itachukua hatua kali, ili alipe deni hilo.”
Hata hivyo, Minde  hakuweka wazi kuwa hukumu ya kwanza ilisomwa lini kwa maelezo kuwa, yeye hakuwapo wakati hukumu hiyo ilipotolewa.

Kwa upande wa Benki ya Azania inayomdai Shellukindo, haikuwa tayari kueleza kiasi cha fedha inachomdai wala mwenendo wa kesi hiyo huku wasemaji wa benki hiyo wakielezwa kuwa kwenye vikao kwa muda mrefu.

“Ni kweli hiyo kesi ipo, lakini mimi siyo msemaji. Kwa sasa wasemaji wa benki wako kwenye kikao cha muda mrefu, labda ufuatilie huko huko mahakamani ” alisema mmoja wa watumishi wa benki hiyo anayefanya kazi katika kitengo cha sheria ambaye hakutaka kutaja jina lake.

Shellukindo ajibu
Alipotakiwa kuzungumzia kesi yake hiyo, Shellukindo alisema hana taarifa kwamba mahakama imemtaka afike mahakamani hapo Machi 7 kusikiliza kesi hiyo.

"Mimi sina taarifa yoyote kwamba natafutwa," alisema Shellukindo akielezea kushangazwa na jinsi jambo hilo linavyopewa umuhimu mkubwa na vyombo vya habari kwa kile alichosema, "We ni mwandishi wa kumi unanipigia kuniulizia juu ya jambo hilo."

Alikiri kuwa ni kweli ana deni analodaiwa na benki hiyo na kwamba, suala hilo siyo la ajabu kwa sababu ni Watanzania wengi wamekopa benki na wanadaiwa hivyo anashangaa kuona yeye kukopa imekuwa ajabu.

Hata hivyo, alitafsiri suala hilo kuwa ni mchezo unaochezwa na maadui zake kisiasa kwa lengo la kumchafua na kushusha heshima yake mbele ya jamii.

Shellukindo alienda mbali akiwatuhumu baadhi ya waandishi wa habari wanaolifuatilia suala hilo kwamba wamehongwa ili kumchafua."Siyo ajabu sasa watakuja wachunguze mimi na mume wangu tuna ndoa au la," alilalamika Shellukindo.
                                       Chanzo na mwananchi

0 comments:

Post a Comment

Mr.Mputa

You are welcome in this blog you ca get us through..
Mobile+255717962720
+255767962720
Njombe Iringa Tanzania

TANGAZO

Karibuni katika Blog ya Jiliwaze hapa utapata mambo mbali mbali yakufunza na kuonya na kama unahitaji kutengenezewa email,facebook ac,page ama blog wasiliana nasi kupitia.. Phone:0717962720/0767962720 Email:mputae@yahoo.com :mputae@rocketmail.com

Popular Posts