Tuesday, February 28, 2012


Kikosi cha Taifa Stars.
Na Wilbert Molandi
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen, amesema kikosi chake kipo tayari kuivaa Msumbiji leo na wachezaji wake wote wamedhamiria ushindi.
Stars itajitupa dimbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kucheza na timu hiyo katika michuano ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2013) zitakazofanyika Afrika Kusini.
Akizungumza na Championi Jumatano,  Poulsen alisema kila kitu cha muhimu kuelekea kwenye mchezo huo kimeshakamilika na kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mchezo huo.
Poulsen pia amefurahia ujio wa kiungo wake, Nizar Khalfan, ambaye alikuwa bado hajajiunga na kikosi hicho kutokana na kukabiliwa na majukumu katika timu yake ya Philadelphia Union ya Marekani.
Aliongeza kuwa, hadi sasa kikosi chake hakina majeruhi yeyote hali inayompa matumaini ya kutumia vyema uwanja wa nyumbani unaoingiza mashabiki 60,000.
Naye kocha wa timu ya taifa ya Msumbiji, Black Mambas, Gert Engels, raia wa Ujerumani, amesema ameshaijua vizuri Stars kupitia mikanda ya video, hivyo yupo tayari kwa mapambano.
                                  Chanco na globalpublishers

0 comments:

Post a Comment

Mr.Mputa

You are welcome in this blog you ca get us through..
Mobile+255717962720
+255767962720
Njombe Iringa Tanzania

TANGAZO

Karibuni katika Blog ya Jiliwaze hapa utapata mambo mbali mbali yakufunza na kuonya na kama unahitaji kutengenezewa email,facebook ac,page ama blog wasiliana nasi kupitia.. Phone:0717962720/0767962720 Email:mputae@yahoo.com :mputae@rocketmail.com

Popular Posts