Friday, February 24, 2012


Posted by GLOBAL on February 24, 2012 at 11:00am 0 Comments

MATESO ya mapenzi ndiyo yanayoongoza kwa maumivu zaidi pengine kuliko kitu kingine chochote. Kuna watu watanishangaa, wanaweza kujiuliza; Vipi kuhusu fedha? Ndugu zangu, fedha haina thamani ya mapenzi.
Siamini kama kuna kitu cha kulinganisha na mapenzi. Ni heri uibiwe milioni ishirini, utaumia, utalia, utahuzunika lakini baadaye utatulia na kutafuta nyingine. Si kumfumania mkeo akiwa na rafiki yako kipenzi kitandani.
Ni rahisi sana kufikia maamuzi mabaya, hatari ambayo ama yatakupeleka jela au utaishia kujiua! Maumivu ya mapenzi ni mabaya sana rafiki zangu. Yes! Ndiyo maana hapa katika Let’s Talk About Love tunazungumza.
Hapa ndiyo sehemu maalumu ya kujadiliana na kupeana angalau kinga ili mapenzi yasiwe chanzo cha maumivu katika maisha yetu. Rafiki zangu, tunajadili matokeo ya sikukuu ya wapendanao.
Naamini kuna ambao…

MATESO ya mapenzi ndiyo yanayoongoza kwa maumivu zaidi pengine kuliko kitu kingine chochote. Kuna watu watanishangaa, wanaweza kujiuliza; Vipi kuhusu fedha? Ndugu zangu, fedha haina thamani ya mapenzi.
Siamini kama kuna kitu cha kulinganisha na mapenzi. Ni heri uibiwe milioni ishirini, utaumia, utalia, utahuzunika lakini baadaye utatulia na kutafuta nyingine. Si kumfumania mkeo akiwa na rafiki yako kipenzi kitandani.
Ni rahisi sana kufikia maamuzi mabaya, hatari ambayo ama yatakupeleka jela au utaishia kujiua! Maumivu ya mapenzi ni mabaya sana rafiki zangu. Yes! Ndiyo maana hapa katika Let’s Talk About Love tunazungumza.
Hapa ndiyo sehemu maalumu ya kujadiliana na kupeana angalau kinga ili mapenzi yasiwe chanzo cha maumivu katika maisha yetu. Rafiki zangu, tunajadili matokeo ya sikukuu ya wapendanao.
Naamini kuna ambao hawataki hata kusikia nikisema neno hili, maana wana vidonda. Wamejeruhiwa, hawana hamu kabisa na siku hiyo kwa vile imewaharibia maisha yao.
Ndugu yangu, jipe moyo, zipo njia ambazo kwa kiasi kikubwa zitakusaidia sana kukupa moyo na kukufanya upige hatua nyingine katika maisha yako ya kiuhusiano.

FUATILIA HAYA...
Rafiki yangu mpendwa, inawezekana unajua ni wapi mpenzi wako alipokosea au ni wapi ulikosea, hadi ikatokea siku hiyo kuwa mbaya kwako.
Hapa nitakupa dondoo chache ambazo ukizifuatilia kwa makini utagundua kuwa mpenzi wako alikuwa na wewe kweli au alikuwa na mambo yake. Sikia nikuambie, inawezekana kabisa ukawa upo na mtu kwa muda mrefu sana, lakini akawa hayupo na wewe kiakili!
Ana mambo yake tofauti kabisa. Hebu angalia hivi vipengele hapa chini ujifunze jambo.

Furaha
Kama ulitoka na mpenzi wako, halafu akawa hana furaha ujue kuna tatizo. Ni wazi kwamba alitoka na wewe kwa lengo la kukamilisha tu ratiba. Hakuwa na amani kutoka na wewe. Kwa maneno mengine ni kama ulikuwa unambana tu.
Kwa bahati mbaya, hulazimisha tabasamu mara kadhaa, ukimwuliza sababu za kutokuwa na furaha, atakataa, ukimlazimisha sana, atakuambia kwamba hajisikii vizuri. Hilo ndilo jibu lake.

Umakini
Ukiwa na mtu ambaye anaonesha umakini sana kwa kila kitu unatakiwa kumtilia mashaka. Muda mwingi anaonekana hataki kukukosea, lakini pamoja na juhudi hizo, lazima mwisho atafanya kitu cha tofauti.
Anajua wazi ana mambo yake, ndiyo maana anajitahidi kuwa makini kwa kila hatua, lakini itawezekanaje wakati anatafutwa na mpenzi mwingine?

Wasiwasi
Kama ulishuhudia akiwa na wasiwasi sana, ujue pia kuna tatizo. Hana amani na muda wote anaonekana kuwa na wasiwasi na kila anachokifanya.
Atakuwa makini sana na simu yake, hatapokea ukiwa naye, kama akifanya hivyo basi mazungumzo yake yalikuwa ya mkato na ni kama anamzungumzisha mtu wa upande wa pili ambaye ndiye aliyepiga simu. Umenisoma?

Ratiba za ghafla
Kimsingi hakupenda sana kutoka na wewe kwa hiyo ama atatafuta njia ili aondoke au sababu ya ghafla. Kwa sababu tayari ana ratiba zake, si ajabu alishampanga mtu ampigie simu na ajifanye kwamba kuna dharura muhimu inayomhitaji.
Upo naye mahali mmetulia, ghafla unashangaa anapigiwa simu, halafu mara anaomba hudhuru – ujue unaibiwa!


NI WAKATI WA KUJIFUNZA
Yapo matukio mengi sana marafiki, kuna ambao wapenzi wao hawakutokea kabisa. Achilia mbali kutopatikana, bali hata zawadi hawakutuma. Hili ni tatizo.
Wapo walioachwa na maumivu makubwa, kuna waliowafumania wenzi wao. Vyovyote iwavyo, ninachotaka kukifafanua hapa ni maumivu ambayo mtu anayapata katika siku muhimu kama hiyo.
Rafiki zangu, yote kwa yote, kikubwa hapa ni kujifunza na kukubali kwamba uliteseka. Mateso ya siku moja pengine yanaweza kuwa tiba yako ya moja kwa moja.
Ungejuaje kama mpenzi wako ni msaliti kama si Valentine? Ungefahamu vipi kama mwenzi wako hana mapenzi ya dhati kwako kama usingeona tofauti siku hiyo?
Kubali matokeo, yawe funzo kwako.

THAMINI MOYO WAKO
Achana na utumwa, kama mtu ana kasoro hasa za uaminifu, huna sababu ya kuendelea kuutesa moyo wako kwa kumng’ang’ania msaliti.
Thamini moyo wako, acha kuunyanyasa. Ni wako wa kuchukua hatua baada ya kujifunza kwa siku moja tu! Ameshindwa kukuthamini katika siku muhimu ya wapendanao, ni lini atakupa heshima?
Fumbua macho ndugu yangu. Usijitese mwenyewe. Penzi la kweli lipo, huyo hakuwa wako, msubiri ajaye. Hayupo mbali, wala hayupo karibu, lakini anakuja! Amini hivyo. Nimesema mara nyingi sana, kuanza upya si ujinga.

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia magazeti ya Global Publishers. Ameandika vitabu vya True Love, Let’s Talk About na Who is your Valentine?, vilivyopo mitaani.

0 comments:

Post a Comment

Mr.Mputa

You are welcome in this blog you ca get us through..
Mobile+255717962720
+255767962720
Njombe Iringa Tanzania

TANGAZO

Karibuni katika Blog ya Jiliwaze hapa utapata mambo mbali mbali yakufunza na kuonya na kama unahitaji kutengenezewa email,facebook ac,page ama blog wasiliana nasi kupitia.. Phone:0717962720/0767962720 Email:mputae@yahoo.com :mputae@rocketmail.com

Popular Posts