Monday, February 20, 2012


Posted by GLOBAL on February 20, 2012 at 9:30am 1 Comment
Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Kina baba, Nderitu Njoka (kulia) akimfariji bw. Francis Muchiri aliyelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mukurwe baada ya kujeruhiwa na mkewe.  [Picha: Job Weru/Standard]
Wanaume nchini Kenya wanapanga kugomea vyakula vya mabibi zao kwa siku sita kutokana  na kuongezeka kwa visa vya wanawake kuwapiga mabwana zao.

Badala yake wanaume watakuwa wakila mahotelini na magengeni

Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Kina baba, Nderitu Njoka amesema mgomo huo wa siku sita una lengo la kuwashinikiza wanawake kukoma kuwanyanyasa na kuwapiga waume zao.

Kiongozi huyo amesema kuanzia leo Jumatatu ataanza kampeni ya kuwashawishi akina baba kula mahotelini badala ya majumbani mwao.

Mwenyekiti huyo wa maendeleo ya wanaume alikuwa akizungumza katika…
Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Kina baba, Nderitu Njoka (kulia) akimfariji bw. Francis Muchiri aliyelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mukurwe baada ya kujeruhiwa na mkewe.  [Picha: Job Weru/Standard] Wanaume nchini Kenya wanapanga kugomea vyakula vya mabibi zao kwa siku sita kutokana  na kuongezeka kwa visa vya wanawake kuwapiga mabwana zao.
Badala yake wanaume watakuwa wakila mahotelini na magengeni
Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Kina baba, Nderitu Njoka amesema mgomo huo wa siku sita una lengo la kuwashinikiza wanawake kukoma kuwanyanyasa na kuwapiga waume zao.
Kiongozi huyo amesema kuanzia leo Jumatatu ataanza kampeni ya kuwashawishi akina baba kula mahotelini badala ya majumbani mwao.
Mwenyekiti huyo wa maendeleo ya wanaume alikuwa akizungumza katika hospitali kuu ya mjini Nakuru huko Rift Valley ambako alikuwa amekwenda kumliwaza baba mmoja ambaye amelezwa humo kutokana na kipigo alichopewa na mkewe.

Baba huyo akizungumza kwa uchungu hospitalini alisema mkewe alimuita nyumbani ili akachukue pesa kabla ya kumfungia chumbani na kumtandika.

Kwa mujibu wa bwana Nderitu Njoka, mkoa wa kati nchini Kenya ndio unaongoza kwa idadi ya akina baba wanaopigwa na bibi zao.

Katika mkoa huo wa kati wanaume karibu nusu milioni wameripoti kutandikwa.
Chama hicho cha wanaume kimedai kuwa kuna wanaume ambao wanalazimishwa kufuo nguo za wake zao.

Wengine pia wamedai kunyimwa tendo la ndoa na mabibi zao.
Jijini Nairobi wanaume ambao huona kivumbi kutoka kwa wake zao ni laki tatu.

Lakini baadhi ya akina mama kutoka mkoa huo wanasema akina baba ndio wa kulaumiwa kwa kushindwa na majukumu yao ya kifamila.
Wanasema wanaume wangi wamekuwa waume suruali tu.

Hata hivyo wengi wanasubiri kuona kama kweli mgomo huo utafaulu, na ni wanaume wangapi walio na pesa za kwenda kula hotelini badala ya kula majumbani mwao.
CHANZO: BBC SWAHILI

0 comments:

Post a Comment

Mr.Mputa

You are welcome in this blog you ca get us through..
Mobile+255717962720
+255767962720
Njombe Iringa Tanzania

TANGAZO

Karibuni katika Blog ya Jiliwaze hapa utapata mambo mbali mbali yakufunza na kuonya na kama unahitaji kutengenezewa email,facebook ac,page ama blog wasiliana nasi kupitia.. Phone:0717962720/0767962720 Email:mputae@yahoo.com :mputae@rocketmail.com

Popular Posts