Thursday, February 5, 2015

Na Musa Mateja
EXCLUSIVE!
Kile kisa cha mtalaka wa mwimba taarab mahiri Bongo, Aisha Ramadhani
Nkongo ‘Isha Mashauzi’, Jumanne Hassan ‘Tevez’ kuteswa na kudhalilishwa
nchini Afrika Kusini kisa kikidaiwa ni kudhulumu mzigo wa
wafanyabiashara wenzake kimeingia awamu nyingine!
Majeraha ya mgongoni aliyopata, Jumanne Hassan ‘Tevez’ wakati wa kuteswa.
Kwa mara ya kwanza Gazeti Pendwa la Amani Tanzania limeweza
kuzungumza na Tevez kwa dakika arobaini na tano kutokea nchini humo
ambako anauguza majeraha.


KWANZA SIKU YA TUKIO
Kabla Tevez hajasimulia
kilichompata na hali yake kwa sasa, ni muhimu kukumbuka kuwa, tukio hilo
ambalo lilikuwa habari ya Jiji la Dar es Salaam, lilijiri mwishoni mwa
wiki iliyopita ambapo picha zake zilizagaa zikimuonesha akiwa amefungwa
kamba huku mwili wake ukiwa umetapakaa damu na majeraha kadhaa.


AMANI LAMSAKA
Kwa vile habari za tukio hilo
ziliandikwa na baadhi ya vyombo vya habari bila kupata balansi (uwiano)
na Tevez mwenyewe, Amani liliingia kazini kumsaka mhanga huyo usiku na
mchana.


MSIKIE SASA
Akizungumza kwa hisia kali na gazeti hili juzi, Februari 3, mwaka huu kutoka Mji wa Durban, Afrika Kusini, Tevez alisema:

“Kusema ukweli tukio lililonikuta watu huko nyumbani (Bongo)
wanalitafsiri tofauti sana. Nimesikia kwamba wanasema eti nilidhulumu
mzigo wa mtu, ndiyo maana niliteswa! Si kweli.”
‘Tevez’ akiwa salama nyumbani kwake.
UKWELI NI UPI?
“Ishu iko hivi, mwenyeji wangu hapa Durban, anaitwa Ibra, ndiye ambaye alinipokea siku nilipotua hapa.
“Huyu bwana inaonekana  ni tamaa. Aliniundia njama, aliita wenzake na kuniteka kisha kunitesa sana wakidhani nina pesa nyingi.
“Niliteswa sana kwa kweli. Kama mlivyoona picha. Nilidhalilishwa sana, lakini katika yote ukweli sijadhulumu mzigo wa mtu.”


ULICHOPOTEZA KATIKA UTESWAJI
 “Katika mateso
yangu, walifanikiwa kunipora Dola za Marekani elfu 14 (kama shilingi
milioni 22) na Randi za Afrika Kusini elfu 3 (shilingi 480,000) zikiwemo
simu zangu mbili aina ya Samsung na Nokia ambazo nilikuwa nazitumia
sana kuwasiliana na watu wangu muhimu.”


HAIKUWA KAZI RAHISI
Tevez akazungumzia jinsi
jamaa walivyomkamata: “Jamaa siku wananiteka usiku kiukweli nilipambana
nao sana hadi wanafikia hatua ya kunizidi nguvu na kunifunga kamba.
Nilikuwa nimewachapa kwelikweli ila kwa vile walikuwa wengi na walikuwa
wakitumia silaha nilijikuta nikiishiwa nguvu baada ya kunipiga na kitu
kizito kichwani nikapoteza fahamu, nilipojitambua ndiyo nikakuta
wamenifunga kamba.”


KINACHOKUUMA NINI?

“Tukio linaloniuma zaidi ni yule jamaa ambaye anaonekana katika picha
amekaa jirani na mimi, hana shati. Alinichoma pasi mgongoni, namchukia
sana lakini nimemwachia Mungu.”
‘Tevez’ akiwa na mwanaye.
KUHUSU KUKATWA NYETI, KUFANYIWA KITU MBAYA

Tevez: “Nasikia watu huko Tanzania wanazusha eti nimekatwa nyeti, si
kweli kabisa. Mimi nimepigwa na kuchomwa pasi wala hakuna kitu kama
hicho zaidi ya kunichoma na pasi.
“Nimesikia wengine wanasema
nimetobolewa macho, huo ni uzushi wa watu tu! Mimi niko safi na hali
yangu ya kiafya inaendelea vizuri.”


SABA WAMEKAMATWA
Tevez tena: “Nashukuru sana
serikali ya huku wameweza kunisaidia kwani mpaka sasa ninapoongea na
wewe Musa Mateja hawa jamaa wamekamatwa saba.
“Jana (Jumatatu)
walifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya kunishambulia na kupora
fedha. Wanatarajiwa kurejea tena mahakamani baada ya siku 7, ingawa
nimeambiwa kesho (jana Jumatano) wataletwa Polisi Central ya huku kwa
ajili ya mimi kuwatambua zaidi.”


BONGO LINI TEVEZ?
“Bongo natarajia kurudi
Alhamisi (leo) au Ijumaa (kesho) kama mambo yangu yatakuwa kwenye mstari
ila pia sasa hivi natarajia kuwasiliana na balozi wetu ili nijue kama
ana taarifa zangu na namna ambavyo ataweza kunisaidia kama kiongozi
wangu.”


HALI YAKO KWA SASA
“Kusema ukweli naendelea
vizuri ni majeraha tu ambayo hata hivyo yanakauka. Ila hili la pasi
mgongoni ndiyo  linasumbua kwa mbali, lakini naamini litakaa sawasawa.”

                                         Na Globel Publishers

0 comments:

Post a Comment

Mr.Mputa

You are welcome in this blog you ca get us through..
Mobile+255717962720
+255767962720
Njombe Iringa Tanzania

TANGAZO

Karibuni katika Blog ya Jiliwaze hapa utapata mambo mbali mbali yakufunza na kuonya na kama unahitaji kutengenezewa email,facebook ac,page ama blog wasiliana nasi kupitia.. Phone:0717962720/0767962720 Email:mputae@yahoo.com :mputae@rocketmail.com

Popular Posts