Monday, February 20, 2012


Posted by GLOBAL on February 20, 2012 at 11:13am 2 Comments
Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
  -Asema ndie mwenye majibu sahihi ya ugonjwa

  -Naye akata, asema suala hilo halina tija kwa polisi

  -Waziri Sitta naye awashukia polisi kwa kupotosha

  -Dk. Mwakyembe aenda India kuendelea na matibabu

Sakata la madai kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ugonjwa wake umetokana kulishwa sumu limewagawa viongozi wa Jeshi la Polisi Nchini na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Wiki iliyopita Jeshi hilo kupitia Mkurugenzi wake wa Upelelezi Makosa ya Jinai (DCI), Kamishina Robert Manumba, lilisema kuwa wakati wa  uchunguzi wake, liliiuliza Wizara hiyo kuhusu madai hayo na kuelezwa kuwa ugonjwa wa Dk. Mwakyembe hauna uhusiano na kulishwa sumu kama inavyoelezwa na baadhi…
Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
  -Asema ndie mwenye majibu sahihi ya ugonjwa
  -Naye akata, asema suala hilo halina tija kwa polisi
  -Waziri Sitta naye awashukia polisi kwa kupotosha
  -Dk. Mwakyembe aenda India kuendelea na matibabu
Sakata la madai kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ugonjwa wake umetokana kulishwa sumu limewagawa viongozi wa Jeshi la Polisi Nchini na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Wiki iliyopita Jeshi hilo kupitia Mkurugenzi wake wa Upelelezi Makosa ya Jinai (DCI), Kamishina Robert Manumba, lilisema kuwa wakati wa  uchunguzi wake, liliiuliza Wizara hiyo kuhusu madai hayo na kuelezwa kuwa ugonjwa wa Dk. Mwakyembe hauna uhusiano na kulishwa sumu kama inavyoelezwa na baadhi ya watu.
Jana NIPASHE liliwasiliana na Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Haji Mponda kutaka kujua kama wizara yake ilitoa taarifa kwa Jeshi hilo wakati wa uchunguzi wa madai hayo na ni ile iliyotoka kwa madaktari wanaomtibu Mwakyembe katika Hospitali ya Andraprasta Apollo iliyopo mji wa Chinai nchini India.
Dk. Mponda hakutaka kulitolea maelezo ya kina suala hilo kwa sababu  hakukanusha wala kuthibitisha badala yake alilitaka NIPASHE kuwasiliane Manumba mwenyewe kwa madai kuwa ndiye anaweza kutoa majibu sahihi kama ripoti ya ugonjwa wa Dk. Mwakyembe aliipata toka wizarani hapo au la.
“Wasiliana na DCI (Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai), ata-‘confem’ na kufafanua zaidi suala hili, sisi kama wizara hatuwezi kuelezea zaidi mambo haya,” alijibu kwa ufupi.
NIPASHE lilipotamtafuta Manumba, alisema Jeshi hilo haliwezi kuendelea kulumbana katika sakala la ugonjwa wa Dk. Mwakyembe kwa sababu kwanza siyo heshima na pia halina tija.

Alisema uchunguzi  ulikamilika na jalada la upelelezi litapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP),  hivyo itakavyoamuliwa kama suala hilo liende mahakamani wataitwa mashahidi ambao watatoa ushahidi.

“Mimi siyo Daktari, kama suala hili litaamuliwa na DPP liende mahakamani wataitwa mashahidi kueleza, lakini kimsingi hakuna sababu ya kuendelea kulumbana katika sakata hili,” alisisitiza Manumba.

Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa iliyopita, Manumba alisema katika uchunguzi wao waliwasiliana na Wizara hiyo ili kupatiwa taarifa kuhusiana na ripoti ya ugonjwa wa Dk. Mwakyembe kama inaonyeshwa alilishwa sumu au la.

Hata hivyo, Manumba alisema wizara hiyo iliwajulisha kuwa maradhi ya Dk. Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela (CCM) hayahusiani na kulishwa sumu.

Kwa upande wake, Dk. Mwakyembe juzi alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akielezea kusikitishwa na tamko la Manumba akisema  jeshi hilo linaonyesha ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko lake.

Alisema jeshi hilo limejiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima uliopita halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kuelewa au kuchunguza madai hayo bali na kuyafanyia mzaha kupitia magazetini.

Alisema msimamo polisi umemkera hasa kutokana na hali aliyonayo ya ugonjwa, akibainisha kuwa umeingilia mchakato wa matibabu yake na uchunguzi wa kina kuhusu kiini cha kuugua.

Matibabu ya Dk. Mwakyembe yanaendelea kwenye hospitali hiyo .

Alisema inashangaza kuona polisi kupitia kwa Manumba, inaelezea hali ya afya yake na kuhitimisha `kienyejienyeji’ kuwa hakulishwa sumu ila anaumwa ugonjwa wa ngozi bila kufafanua umesababishwa na nini.

Dk. Mwakyembe alisema anapata tabu kuamini kama Manumba na maofisa wenzake waliisoma taarifa halisi ya matatibabu yake au walisoma taarifa nyingine.

Alisema kama viongozi hao wa polisi waliisoma taarifa hiyo wenyewe au walisomewa, kwa nini alichokisema Manumba kwa waandishi wa habari hakifanani na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya Hospitali ya Apollo anakotibiwa.

“Taarifa ya hospitali ya Apollo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow (ute ulio ndani ya mfupa) kinachochochea hali niliyonayo,” alisema Dk. Mwakyembe.

AENDA INDIA

Wakati viongozi hao wakieleza hayo, taarifa zinaeleza kuwa Dk. Mwakyembe ameondoka nchini jana kuelekea India kwa ajili ya kuendelea na matibabu katika Hospitali ya Andraprasta Apollo.

 Taarifa hizo zilidai kuwa Dk. Mwakyembe atakuwa nchini humo kwa siku chache kulingana na uchunguzi atakaofanyiwa na madaktari wanaomtibu.

Dk. Mwakyembe aliugua ugonjwa wa ngozi Oktoba 9, mwaka jana na kupelekwa nchini humo kwa matibabu na kulazwa katika Hospitali hiyo iliyoko mjini China na kurejea nchini Desemba 11 mwaka jana.

SITTA: SISEMI UONGO

Kwa mara nyingine, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ameendela kusisitiza kwamba ugonjwa unaomsumbua Dk. Mwakyembe unatokana na kulishwa sumu.

Alisema kwamba hoja ya jeshi hilo kusema kuwa suala hilo linahitaji ushahidi ni kuupotosha umma ili usielewe nini kinachomsumbua kiongozi huyo.

Akizungumza katika uzinduzi wa asasi ya kiraia ya vijana wa kanisa katoliki mkoani Tabora (VITAL), uliofanyika kwenye ukumbi wa Askofu Mkuu Marco Mihayo, alisemakama waziri hawezi kusema uongo kuhusu jambo hilo.

Alisema jeshi hilo limekuwa likipotosha umma kwa kukanusha kwamba Dk. Mwakyembe hajalishwa sumu ingawa yeye mwenyewe anaushahidi wa kutosha kuhusu jambo hilo.

“Mimi nitapigana hadi siku ya mwisho kutetea wanyonge na ninashangaa kuelezwa kwamba nimeshtakiwa kwa kupotosha umma kwa kusema kwamba Dk. Mwakyembe amelishwa sumu na kwa taarifa yako Baba Askofu nimeelezwa jalada langu limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) ili nishitakiwe,” alisema Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM).

Alilishutumu jeshi hilo kutokana na tabia ya kuhujumu watu na kusisitiza kuwa tabia hizo ni za ‘kijambazi’ ambazo zinaweza kuhatarisha hali ya usalama na maisha ya watu wanaozuliwa mashitaka kama hayo yanayomkabili.

Akizungumza kuhusu ufisadi, Sitta, alisema amekuwa mstari wa mbele kuupinga kwa nguvu zote na kwamba atahakikisha anapigana kufa na kupona kupambana na watu wanaojilimbikizia mali kwa kutumia madaraka yao.

0 comments:

Post a Comment

Mr.Mputa

You are welcome in this blog you ca get us through..
Mobile+255717962720
+255767962720
Njombe Iringa Tanzania

TANGAZO

Karibuni katika Blog ya Jiliwaze hapa utapata mambo mbali mbali yakufunza na kuonya na kama unahitaji kutengenezewa email,facebook ac,page ama blog wasiliana nasi kupitia.. Phone:0717962720/0767962720 Email:mputae@yahoo.com :mputae@rocketmail.com

Popular Posts