Posted by GLOBAL on February 18, 2012 at 7:00am
3 Comments
0 Likes

Sifael Paul na Mtandao
Wakati leo mwili wake ukitarajiwa kuhifadhiwa katika nyumba ya milele huko Newark New Jersey, Marekani, imethibitika kuwa, saa 24 kabla ya kukutwa na mauti, mwanamuziki Whitney Elizabeth Houston, alipigana, Risasi Jumamosi limeinyaka.
Kwa mujibu wa mtandao wa Bossip wa nchini humo, ishu hiyo ilijiri usiku
wa Ijumaa wiki iliyopita ambapo staa huyo wa muziki wa Pop, RnB na Soul
aliyeaga dunia Februari 11, 2012, alizua bonge la varangati katika
klabu moja maarufu huko Los Angeles (haikutajwa).…
Sifael Paul na Mtandao
Wakati leo mwili wake ukitarajiwa kuhifadhiwa katika nyumba ya milele huko Newark New Jersey, Marekani, imethibitika kuwa, saa 24 kabla ya kukutwa na mauti, mwanamuziki Whitney Elizabeth Houston, alipigana, Risasi Jumamosi limeinyaka.
Kwa
mujibu wa mtandao wa Bossip wa nchini humo, ishu hiyo ilijiri usiku wa
Ijumaa wiki iliyopita ambapo staa huyo wa muziki wa Pop, RnB na Soul
aliyeaga dunia Februari 11, 2012, alizua bonge la varangati katika klabu
moja maarufu huko Los Angeles (haikutajwa).
Hata
hivyo, habari hiyo haikueleza chanzo cha ugomvi huo na aliyekuwa
anapigana naye zaidi ya kutoa picha zilizomuonesha Whitney
akipandishiana na walinzi waliokuwa wakimshika kumtoa nje ya klabu.Katika purukushani hiyo, mguu wa kushoto wa Whitney ulionekana ukichuruzika damu ambapo aliongozwa na walinzi wake akapanda kwenye gari lake na kutimka eneo hilo.
Wakati
huo huo ratiba ya mazishi ya staa huyo inaonesha mwili utaagwa kwenye
Kanisa ambalo msanii huyo alianzia uimbaji la New Hope Baptist lililopo
Newark New Jersey huku wakialikwa watu maalumu wapatao 300 tu.Ilielezwa kuwa katika mwaliko huo wa mazishi, aliyekuwa mume wa Whitney kati ya mwaka 1992 hadi 2007, Bobby Brown hakualikwa huku mwenyewe akitaka kumuona mwanaye waliyezaa pamoja, Bobbi Kristina.

0 comments:
Post a Comment