Zimbabwe yaondolewa vikwazo na EU
Muungano
wa Ulaya umewaondolea vikwazo baadhi ya maafisa wakuu wa serikali ya
Zimbabwe, ingawa utaendelea kushikilia mali ya rais wa nchi hiyo Robert
Mugabe pamoja na washirika wake wa karibu.
Kwa
mujibu wa muungano huo, vikwazo vya usafiri dhidi ya mawaziri wawili
viliondolewa ili kushinikiza serikali kuharakisha mchakato wa mageuzi.
Lakini
msemaji wa chama cha rais Robert Mugabe,alipinga hatua hiyo akitaja
vikwazo hivyo kama vinavyokiuka sheria, vyenye misingi ya ubaguzi wa
rangi na vitakavyoathiri uchumi wa nchi.
Muungano
huo pia uliondoa takriban kampuni ishirini za serikali kwenye orodha
hiyo ambazo muungano huo ulidai kuwa zilisaidia kufadhili vurugu
nchini Zimbabwe.
Ingawa
Zimbabwe imepiga hatua katika mchakato wa kuunda katiba mpya, na
kuimarisha uchumi, Muungano huo ungali na wasiwasi ikiwa ahadi
zilizowekwa baada ya uchaguzi uliokumbwa na vurugu mwaka 2008, ikiwemo
ahadi za kufanyia mabadiliko idara ya polisi hazijaweza kutimizwa.
0 comments:
Post a Comment