"KIJANA ACHOMA KISU UTUMBO WATOKA NJE"
mpenzi
mdao wa mtandao huu kwanza naomba radhi kwa picha hizi za
kusikitisha ila ndio hali halisi ya mambo inatisha sana 
Kijana
kizito Kimeya (28) mkazi wa kijiji cha Mkoga kata ya Isakalilo
Manispaa ya Iringa akiwa Hospitali ya mkoa wa Iringa kupatiwa
matibabu baada ya kuchomwa kisu na utumbo wake kutoka nje

Miguu ikiwa imekatwa katwa mapanga na wauwaji hao ambao hawakufanikiwa kutimiza azmayao

hapa utombo ukiwa nje baada ya kuokolewa na afisa mtendaji wa kata hiyo ya Isakalilo Iringa mjini
Ni
vigumu kuamini kama kweli kuna binadamu na wanywa damu ila
kutokana na matukio kama hayo ndipo unaweza kuamini kuwa wapo
binadamu na wanywa damu baada ya watu wanne ambao majina yao
yametajwa na kijana huyo kudaiwa kumchoma visu kijana huyo pichani
baada ya kumfuma akiiba mahindi ya mabichi maarufu kama Gobo katika
shamba lao Kijana
huyo alichomwa kisu na kucharangwa mapanga na baada ya wahusika
kutenda unyama huo walimchukua na kumweka katika mfuko wa
sarufeti na kujaza mchanga na kisha kumtupa mtoni kabla ya na
kusindwa katika maji kwa masaa zaidi ya matano na baadae maji kusaidia
kuupasua mfuko huo na mchanga wote kumwagika na kijana huyo
kujisaidia kujikokota hadi nje kavu na kukutwa porini siku ya pili
yake majira ya saa 1 usiku na wasamaria wema.
Chanzo: http://www.francisgodwin.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment