JIJINI ARUSHA
Tukio hilo lililovuta umati mkubwa ambalo lilishuhudiwa na shushushu
wetu, lilijiri maeneo ya stendi ya mabasi madogo jijini Arusha, wiki
iliyopita wakati mrembo huyo akiwa na marafiki zake watatu
wakirandaranda kufanya ‘window shopping’.
Mara baada ya kufika eneo
hilo, miss huyo alijikuta akizungukwa na wapiga debe wa daladala na
kuanza kumshushia maneno makali wakimwambia kuwa wamechoshwa kuona nyeti
zao.
AVULIWA
Huku sistaduu huyo akidhani ni kelele za kawaida, wapiga debe hao walimzingira na kuanza kumvua kigauni hicho cheusi.
APEWA KITENGE
Mrembo huyo alipoona mambo yameharibika huku wenzake wakitoka nduki,
alilazimika kukimbilia katika duka moja la nguo maeneo hayo na kuomba
msaada ambapo alisitiriwa kwa kupewa upande wa kitenge kwa msaada wa
trafiki wa kike aliyemuokoa.
Kabla ya kusaidiwa na trafiki mwingine wa kiume, yule wa kike alimshauri kuvaa kitenge hicho na kuondoka eneo hilo.
AKIMBIZWA
Cha kushangaza, wakati anatoka katika duka hilo hali ilizidi kuwa tete
baada ya midume walioonekana kuchoshwa na uvaaji wa nguo fupi kumkimbiza
na kuanza kumvua kitenge hicho hivyo kusababisha vurugu kubwa kiasi cha
matrafiki kadhaa kuingilia kati na kuwatawanya vijana hao.
AJITETEA
Wakati dada huyo akihojiwa na matrafiki hao, alijitetea kuwa
anawashangaa vijana hao kwa kumfanyia vurugu wakati nguo hiyo siyo fupi
na mara nyingi amekuwa akiivaa na kutembea nayo maeneo kama hayo bila
kupata tatizo lolote.
“Afande hii nguo huwa naivaa sana na sijawahi
kupata matatizo yoyote, sijui leo imekuwaje lakini siyo fupi kama
wanavyodai, nimevaa na kitenge lakini bado wananifanyia vurugu,”
alilalamika dada huyo kwa uchungu.
Licha ya dada huyo kuwa katika
mikono ya mmoja wa matrafiki wa kiume, jamaa hao walizidi kumfuatilia
huku wakimrushia maneno makali ya matusi na wakati mwingine kumsukuma.
Baada ya trafiki huyo kuona hali inazidi kuwa mbaya, alisimamisha gari
moja la serikali na kumuombea lifti kwa lengo la kumnusuru kufanyiwa
kitu mbaya.
TUMEWACHOKA
Wakizungumza na gazeti hili juu ya
tukio hilo, ‘machalii’ hao walisema kuwa wamechoshwa na uvaaji mbovu wa
baadhi ya akina dada ambapo sasa wameamua kuwafanyia vurugu hizo mpaka
hapo watakapoacha kuvaa hovyo.
“Tunakushukuru kwa kupiga picha,
wanatuchosha hawa dada zetu, nguo wanazotuvalia barabarani ni za kuvaa
nyumbani tena chumbani lakini wao wanavaa sehemu kama hizi, kuanzia sasa
kazi itakuwa kama hii hadi watakapoacha, dawa yao ni kuwawashia moto,”
alisema mmoja wa wapiga debe hao huku akisapotiwa na wenzake.
Siku
za nyuma mchezo wa kuwavua nguo fupi wanawake ulisaidia kupunguza tabia
ambapo kwa sasa imerejea kwa kasi hivyo ili wanusurike na adha hiyo ya
kuvuliwa hadharani inayoshika kasi, inabidi kuvaa kiheshima. na Global publishers
Monday, September 2, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment