Friday, October 18, 2013

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete aliwasili mjini Njombe jana, Alhamisi, Oktoba 17, 2013, kuanza ziara ya wiki moja kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Njombe.
Miongoni mwa shughuli kubwa ambazo Rais Kikwete atazifanya katika ziara hiyo  ya kwanza tokea Njombe kutangaza kuwa Mkoa, ni kuuzindua rasmi Mkoa huo.
Katika siku yake ya kwanza leo Oktoba 18,  mbali na kuzindua Mkoa wa Njombe pia atazindua Kiwanda cha Chai katika eneo la Ikanga na kuzungumza na wananchi.
Katika ziara hiyo ambako pia Rais Kikwete atatembelea wilaya zote za mkoa huo ambazo ni Njombe, Wanging’ombe, Ludewa na Makete, pia atazindua Chuo cha Veta cha Mkoa.
Aidha, Rais atatembelea na kupata taarifa kuhusu maendeleo ya mradi wa chuma wa Liganga.
na Amani blog

0 comments:

Post a Comment

Mr.Mputa

You are welcome in this blog you ca get us through..
Mobile+255717962720
+255767962720
Njombe Iringa Tanzania

TANGAZO

Karibuni katika Blog ya Jiliwaze hapa utapata mambo mbali mbali yakufunza na kuonya na kama unahitaji kutengenezewa email,facebook ac,page ama blog wasiliana nasi kupitia.. Phone:0717962720/0767962720 Email:mputae@yahoo.com :mputae@rocketmail.com

Popular Posts